UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA
Afisa
Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za
aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel
anayedaiwa kutoroshwa na kueleza kuwa mtu huyo alipatiwa notice ya
kuondoka nchi ambapo Juni 10 mwaka huu aliamriwa kuondoka nchi Juni 13
huku akisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa Kia kama
ilivyoelezwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari
amesema kuwa Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice
ya kuamriwa kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo
ulizingatia taratibu zote za kisheria.
Nanomba alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika
kusini na alikua mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita
na kuwaonya.
Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri
yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi na hivyo kuwataka waajiri
wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchi vinginevyo
watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa hadi sasa wamewachukulia hatua
waajiri watano.
Kwa kipindi cha Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa
kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya
ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.
Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
Pia wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa
nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni