UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA
Jumatatu, 23 Juni 2014
UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA
WASOMI ONDOENI FIKRA ZA KUAJIRIWA-MASSOUD
WASOMI ONDOENI FIKRA ZA
KUAJIRIWA-MASSOUD
Wasomi nchini wametakiwa kuondoa
fikra za kuajiriwa na badala yake wawe wabunifu na kutumia dhana ya
ujasiriamali kujiajiri na kuwaajiri wengine kwani kwa kufanya hivyo watakua
wameongeza pato la taifa.
Hayo yameelezwa Meneja Mauzo
wa Kampuni ya Soda za Pepsi na Mirinda (SBC) ltd,Ali Massoud alipokua
akizungumza katika Maonyesho ya nne ya Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha
Arusha kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani hapa,Massoud amesema kuwa kampuni
nyingi zimekua zikipunguza wafanyakazi kutokana na kukua kwa teknolojia
inayoziba nafasi ya nguvu kazi na kusababisha ufinyu wa nafasi hivyo amewataka
wasomi kuwa na mbinu mbadala ya kujiajiri.
Meneja huyo amewataka
Vijana watengeneze bidhaa na kuanzisha makampuni ili kuondoa fikra za
kuajiriwa.
Mratibu wa Maonyesho hayo
Dr.Janeth Jonathan Marwa amesema kuwa wamekuwa wakiwafundisha Wanachuo
ubunifu wa kijasiriamali ili uweze kuwasaidia kukua kiuchumi kuanzia ngazi ya
mtu mmoja mmoja hadi taifa.
Dr.Janeth amesema kuwa Vijana
wanapaswa kutambua kuwa kazi ipo kwao si wahitimu na kwenda kutafuta kazi bali
waende kuajiajiri na kuajiri wengine.
Mbunifu wa Mavazi (designer) ,Bavuma
Joshua anayetengeneza mavazi kwa kutumia gunia na vitenge amesema kuwa
wanafundishwa kuona mbali zaidi hata pasipoonekana na kufanya vitu vya
kitofauti jambo linalochochea ubunifu ulioko ndani yao.
Bavuma ambaye ni Mwanafunzi wa Mwaka
wa Pili wa Ujasiriamali (Interprenureship) amesema kuwa anatarajia baada ya
kuhitimu chuo hata kwenda kuomba kazi bali atakwenda kuwapa watu kazi kwani
malengo yake pia ni kuwasaidia vijana wasiokuwa na ajira.
Naye Afisa Uhusiano wa Chuo hicho
William Izungo akielezea Maonyesho hayo yaliyohusisha masuala mbali mbali
ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za chakula,samani,utamaduni, sabuni
,ramani za nyumba,amesema kuwa Wanazuoni hao wameonyesha ubunifu na uwezo
mkubwa ambao Mungu amewapatia na anatarajia kuwa wataisaidia jamii kwa ubunifu
wao.
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)