Jumatatu, 7 Julai 2014

MWANA WA MFALME WA JAPAN PRINCE AKISHINO AFURAIA NGOMA ZA KIMASAI,NA WA BARBAIG

Mwana wa mfalme wa Japan Prince Fumihito Akishino akipewa maelezo  mbalimbali

Mwana huyo wa mfalme wa Japan akipewa maelezo
kuhusu shughuli za uhifadhi ndani ya mamlaka ya Ngorongoro katika kutuo cha habari
cha Loduare Gate,

Mwana wa mfalme wa Japan Prince Fumihito Akishino na mkewe Kiko,
wakifurahia ngoma za makabila la Wadatoga (Barbaig) na ile ya Wamasai,
katika eneo la mlango wa Loduare kwenye hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro,
pamoja nao wapo pia maafisa wa mamlaka hiyo, Bruno Kawasange na Adam Akyoo
pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu, Felix Daudi Ntibenda.

Jumatatu, 23 Juni 2014

UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA

UHAMIAJI WAKANUSHA JUU YA MHAMIAJI ALIYEDAIWA KUTOROSHWA
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za  aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa na kueleza kuwa mtu huyo alipatiwa notice ya kuondoka nchi ambapo Juni 10 mwaka huu aliamriwa kuondoka nchi Juni 13 huku akisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa Kia kama ilivyoelezwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice ya kuamriwa kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo ulizingatia taratibu zote za kisheria.
Nanomba alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika kusini  na alikua mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita na kuwaonya.
Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi na hivyo kuwataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchi vinginevyo watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano.
Kwa kipindi cha Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.
Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
Pia  wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini.

WASOMI ONDOENI FIKRA ZA KUAJIRIWA-MASSOUD

WASOMI ONDOENI FIKRA ZA KUAJIRIWA-MASSOUD


Wasomi nchini wametakiwa kuondoa fikra za kuajiriwa na badala yake wawe wabunifu na kutumia dhana ya ujasiriamali kujiajiri na kuwaajiri wengine kwani kwa kufanya hivyo watakua wameongeza pato la taifa.

Hayo yameelezwa Meneja Mauzo wa  Kampuni ya Soda za Pepsi na Mirinda (SBC) ltd,Ali Massoud alipokua akizungumza katika Maonyesho ya nne ya Ujasiriamali katika Chuo kikuu cha Arusha kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani hapa,Massoud amesema kuwa kampuni nyingi zimekua zikipunguza wafanyakazi kutokana na kukua kwa teknolojia inayoziba nafasi ya nguvu kazi na kusababisha ufinyu wa nafasi hivyo amewataka wasomi kuwa na mbinu mbadala ya kujiajiri.
Meneja huyo  amewataka  Vijana watengeneze bidhaa na kuanzisha makampuni ili kuondoa fikra za kuajiriwa.

Mratibu wa Maonyesho hayo Dr.Janeth  Jonathan Marwa amesema kuwa wamekuwa wakiwafundisha Wanachuo ubunifu wa kijasiriamali ili uweze kuwasaidia kukua kiuchumi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi taifa.

Dr.Janeth amesema kuwa Vijana wanapaswa kutambua kuwa kazi ipo kwao si wahitimu na kwenda kutafuta kazi bali waende kuajiajiri na kuajiri wengine.

Mbunifu wa Mavazi (designer) ,Bavuma Joshua anayetengeneza mavazi kwa kutumia gunia na vitenge amesema kuwa wanafundishwa kuona mbali zaidi hata pasipoonekana na kufanya vitu vya kitofauti jambo linalochochea ubunifu ulioko ndani yao.

Bavuma ambaye ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Ujasiriamali (Interprenureship) amesema kuwa anatarajia baada ya kuhitimu chuo hata kwenda kuomba kazi bali atakwenda kuwapa watu kazi kwani malengo yake pia ni kuwasaidia vijana wasiokuwa na ajira.

Naye Afisa Uhusiano wa Chuo hicho William Izungo  akielezea Maonyesho hayo yaliyohusisha masuala mbali mbali ya utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za chakula,samani,utamaduni,sabuni ,ramani za nyumba,amesema kuwa Wanazuoni hao wameonyesha ubunifu na uwezo mkubwa ambao Mungu amewapatia na anatarajia kuwa wataisaidia jamii kwa ubunifu wao.